Changamoto Zinazowakumba Vijana Katika Tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga

 

Jackson Ndung’u Mwangi

Chuo Kikuu Cha Laikipia, Kenya

jigmwas@gmail.com

Ikisiri

Katika ulimwengu wa sasa, kuna mabadiliko chungu nzima yanayoshuhudiwa duniani kote yanasababishwa na masuala anuwai kama vile maendeleo ya kiteknolojia pamoja na utandarithi yanayoathiri pakubwa maisha ya vijana. Hapo nchini, vijana wana umuhimu wa kipekee kwani wanatekeleza majukumu muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi. Isitoshe, idadi ya vijana kote ulimwenguni imeendelea kuongezeka kila uchao na imepiku ile ya wazee.  Kwa hivyo, ni nyema kujadili changamoto zinazowakabili na kupendekeza hatua za kukabiliana nazo. Lengo la utafiti huu lilikuwa ni kuchanganua changamoto zinazowakumba vijanapamojanaathari zake katika ya tamthilia ya Kitumbua Kimeingia MchangayaS.A Mohamed (2000).Mada hiiilichaguliwakwamisingikwambavijanawanakumbwanachangamoto nyingikatikamaishayao zinazowaathiri kwa kiasi cha haja na kutinga juhudi za kuafikia jaala zao.Utafiti huu ulilenga kubainisha changamoto zinazowakumba vijanakatika tamthilia hii na kutambua mbinu ambazo vijana hawa wanazua ili kukabiliana nazo. NadhariayaUhalisiailitumika kwa sababuilionekana kufaa  zaidi kuchanganua  changamoto  zinazowakumba  vijana  kwani changamoto hizi  zina uhalisiamkubwakatikamaishayao. Madhumuniyautafiti huu yalikuwa ni kuchunguzanakueleza namna changamoto za vijana zinavyojitokeza katika tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga na kisha kubainisha hatua zinazochukuliwa kuzitatua changamoto hizo. Utafiti huu ni wa kimaelezo na kiudhamano kwani ulihusisha kuchanganua matini zinazohusiana na mada husika. Sampuli katika utafiti huu iliteuliwa kimakusudi kwani ndiyo ingempa mtafiti data aliyonuia kuipata. Utafiti huu ulijikita katika maktaba ya kitaifa na yale ya vyuo vikuu humu nchini.  Utafitiwetuumebainisha kidakidaki kwambatamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga imesheheniChangamoto nyingi mno zinazowaathiri vijana kamavile dawa za kulevya, dhuluma,anasa,uavyaji mimba,utabaka, athari za tamadunizakigenipamoja nakufanyiwa uamuzi.Aidha, imethihirika wazikuwa vijana wanazua mbinu kabambe za kutatua changamoto zinazowakumba kama vile kutafuta ushauri kutoka kwa wenzao, kutumia wazee na kuwa na ujasiri wa kujitetea dhidi ya wanaowadhulumu pamoja na serikali kukabiliana na walanguzi wa dawa za kulevya. Ni bayana kuwa utafiti huu utaifaa jamii ya wasomi wanaoshughulikia maswala ibuka katika jamii. Inapendekezwa kuwa tafiti za baadaye zitafiti kuhusu nafasi ya vijana katika jamii.

 

Maneno Elekezi: Dhana ya Vijana, Jaala, Changamoto, Athari, Uhalisia

Application Forms
Download Abstract: Changamoto Zinazowakumba Vijana Katika Tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga_Kibabii University Conference Abstract